Monday, 22 May 2017

SABATO

 SABATO

Kutoka 20:8 “Ikumbuke siku ya sabato uitakase”..

Sabato ni neno la kiyunani linalotokana na aneno “shabbath” linalomaanisha pumziko (rest). Neno hili kwa kingereza huitwa Sabbath” linalomaanisha pia maana ile ile pumziko.

Katika juma la uumbaji (mwanzo sura ya 1) Mungu anafanya kazi zake kwa siku siku akiumba vitu vyote vilivyo duniani. Katika siku ya saba yeye mwenyewe (Mungu) anapumzika na kustarehe. Mwanzo 2:1-4 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi. Chimbuko la pumziko letu ni Mungu mwenyewe.

Wana wa Israeli katika safari ya kutoka Misri kwenda Kaanan Mungu anawakumbusha juu ya upendo wake kwao. Na hivyo anawapa taratibu ya namna ambavyo sasa imewapasa kuenenda kwa kicho mbele za Mungu. Katika mlima Sinai Mungu anampa Musa mbao mbili za mawe zikiwa na amri 10. Ambazo zilikuwa katika mgawanyiko wa Amri 4 kwa Amri 6. Zenye amri 4 zilihimiza juu ya upendo wa Mwanadamu kwa Mungu, zenye amri 6 zilihamasisha juu ya upendo wa mwanadamu kwa mwanadamu mwenzake. Ndio maana Yesu anawaambia wanafunzi wake juu ya amri anaelezea kwa ufupi “amri kuu ndio hii umpende Bwana Mungu wako………, nay a pili nayo yafanana nayo mpende jirani yako kama nafsi yako” Mthayo 22:37-40.

Katika amri hizi 10, amri ya 4 huzungumza kwa upana juu ya sabato. Kutoka 20:8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Swali la kujiuliza. Kwanini Mungu anawaambia waikumbuke??? Kukumbuka jambo Fulani maana yake ni kwamba huenda ulisahau, na hata hivyo huwezi ukakumbuka kitu ambacho hakikuwahi kuwepo. Bila shaka habari ya sabato ilikuwepo hata kabla ya wana wa Israeli kwenda utumwani Misri. Lakini kwanini Mungu anawataka waikumbuke sabato je waliisahau kweli? Kumbuka kuwa taifa la Misri halikumtambua Mungu na ndiyo maana Musa alipomuendea Farao kuomba ukubali ili wana wa Israeli waondoke alimuuliza Musa Mungu wenu ni nani? Mwanzo 5:2…. Maana yake ni kwamba wamisri waliabudu miungu Kutoka 12:12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. Kwahiyo wana wa Israeli hawakupata muda wa kumuabudu Mungu wao kwakuwa walitumikishwa.

Mungu anawataka wana wa Israeli waikumbuke sabato na kuitakasa (kutakasa maana yake kuifanya kuwa safi) wasiihalifu, wasiinajisi, wasiidharau (isaya 58:13). Waifanye kuwa siku maalum kama yeye alivyofanya siku ya saba kuwa maalum kwa kupumzika kuitakasa na kuibariki. Mungu anawaamuru wanaisraeli kuzitakasa sabato zake kwakuwa ni ishara kati ya Mungu na wanadamu. Ezekiel 20:12,20 Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, Bwana, ndimi niwatakasaye…… zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. “Sabato ni ishara kati ya Mungu na wanadamu”

JE SABATO ILIKUWA NI KWA AGANO LA KALE PEKEE??

Kumekuwepo na dhana mbali mbali kuwa sabato ilikuwa tu ni kwa ajili ya wayahudi peke yao je Yesu mwenyewe alipokuwa duniani aliitunza sabato?

Luka 4:16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. Marko 6:2 Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake……. Yesu pia alikuwa na kawaida ya kuingia katika sinagogi na kusali siku ya sabato

Je huenda Yesu mwenyewe kwa kifo chake aliibatilisha sabato kwa kuwa twaelewa kuwa sheria za wana wa Israeli nyingi zilikuwa ni kivuli cha msalaba. Mathayo 5:17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Yesu anatangulia kutupa angalizo kuwa yeye hakuja kuitangua torati (sheria) bali kuitimiliza (kuitiisha). Ieleweke kuwa katika mambo yaliyokuwa yakiishia msalabani kwa kifo cha Yesu amri 10 za MUNGU hazimo. Hizi bado ziliendelea kuwepo na bado zipo na zitakuwepo kwakuwa ni agano la milele. Na ni hizi amri ndizo Yesu anatuambia mwenyewe kuwa hakuja kuziondoa bali kutufundisha ushikaji wake. na hivyo amri ya sabato bado iko palepale kama ambavyo amri zingine pia zipo.

Kama Yesu mwenyewe aliitunza sabato na anatuambia mwenyewe kuwa hakuibadilisha sheria je huenda ni mitume ndio waliobadilisha amri ya sabato? Matendo 16:13 Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. Mtume paulo na sila wakiwa makedonia waliitunza sabato na walikutana siku ya sabato kusali. Matendo ya mitume 17:2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu,………… matendo ya mitume 18:4 Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani.. Hata mitume pia waliitunza sabato na Paulo pia alikuwa na desturi ya kutoa mafundisho katika sinagogi kila sabato.

 JE SABATO ITAISHIA TU HAPA DUNIANI?

 Isaya 66:22, 23Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana. hii hutuambia dhahiri kuwa sabato haitaishia tu kutunzwa hapa duniani lakini hata mbinguni watakatifu wa Bwana watajihudhurisha mbele za Bwana panapo sabato naam hata katika nchi tutamwabudu Mungu wetu. kadiri mbingu na nchi zitakavyodumu, sabato itaendelea kuwa ni alama ya uwezo wa Muumbaji


JE SIKU YA SABATO NI LINI HASA? (IJUMAA, JUMAMOSI AU JUMAPILI?)

Kumekuwa na madai mengi sana kuwa sabato iliishia msalabani kitu amabacho si kweli, wengine wanadai biblia haijaweka wazi kuwa ni ipi hasa kweli siku ya sabato kwahiyo ni radhi kusali siku yoyote hata jumanne jumapili ijumaa nk…. Lakini je Biblia inatuambia nini kuhusu siku halisi ya sabato??

Mungu aliumba mbingu na nchi kwa siku 6 na siku ya saba akapumzika maana ilikuwa ni sabato. Mwanzo 2:2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Hii hutuonesha moja kwa moja kuwa siku ya sabato ilikuwa ni siku ya saba. Sasa je siku ya saba hasa ni lini? Kwa kawaida leo hii tunahesabu siku kwa majina ya kiarabu (jumampili, jumatatu, jumanne, jumatano, alhamis, ijumaa na jumamosi) na hii ndio hasa huleta shida kwa wengine hasa kwa kuwa neon mosi humaanisha moja basi wao huchukulia jumamosi kama siku ya kwanza na ijumaa kama siku ya saba. Wengine wao huadhimisha jumapili kama siku ya saba (sabato) kwa kuwa ndio siku ya ufufuo kwahiyo kwao sabato siyo siku ya saba bali ni siku ya ufufuo, lakini wengine pia huadhimisha jumamosi kama siku ya sabato kwa kuwa ndiyo siku ya saba.

Hebu tuangalie ushahidi katika biblia. 

Luka 23:54 Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia. katika sura nzima ya 23 cha kitabu cha luka na vitabu vingine vya injili kama vile marko 15, mathayo 27 na yohana 19 habari ya kifo cha mkombozi wetu zinaelezwa hapo. Biblia takatifu inatuambia kuwa Yesu alipokamatwa kwa kusudi la kuuawa ilikuwa ni siku ya maandalio ya sabato. Maana yake ni kwamba ailikuwa siku moja kuelekea sabato. Kwa lugha nyingine tutakubaliana kuwa ilikuwa ni siku ya sita nayo siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya saba yaani sabato.

Tuangalie pia siku ya ufufuo wake ilikuwa ni lini. 

Luka 24:1 Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari. soma pia mathayo28:1, Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi. soma marko 16:1 na yohana 20:1. Maandiko yote yako wazi kutuonesha kuwa Yesu alifufuka siku ya kwanza ya juma na pia yanasisitiza kuwa ilikuwa ni baada ya sabato… bila shaka yoyote kama tunaikubali biblia tutakubali kuwa ni kweli Yesu Kristo alikufa siku ya sita (maandalio ya sabato) na akafufuka siku ya kwanza (baada ya sabato)

Maadhimisho ya pasaka leo hii pia yaweza kutupatia mwanga kidogo juu ya kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo. Dunia nzima inatambua kuwa Yesu alikufa siku ya ijumaa na kafufuka jumapili. Na kama tukishaelewa kuwa Yesu alikufa ijumaa ambayo ndiyo biblia hutuambia kuwa ilikuwa ni siku ya maandalio ya sabato au siku ya sita ya juma je siku inayofuata ni ipi?? Bila shaka ni JUMAMOSI

Vilevile biblia huweka wazi kuwa Yesu alifufuka siku ya kwanza ya juma ambayo bila shaka ni jumapili nayo yatjwa kama siku baada ya sabato je siku inayotanguliwa na jumapili ni ipi? Hakuna hofu kuwa ni JUMAMOSI. 

Hii hutupatia hitimisho kuwa Yesu alikufa ijumaa iliyokuwa maandalio ya sabato (Jumamosi) na akafufuka jumapili ambayo ilikuwa ni baada ya sabato. Hivyo tunakubaliana kuwa siku ya sabato ambayo BWANA MUNGU alipumzika, ambayo YESU KRISTO aliingia katika sinagogi na ambayo mitume pia walikutana kusali ilikuwa ni JUMAMOSI.


BWANA AKUBARIKI

BY; PETER JEFTER 
0785167164
peterjefter91@gmail.com

TUTAWAONA TENA WAPENDWA WETU


                                TUTAWAONA TENA WAPENDWA WETU TULIOTENGANA NAO
                                                             (WALIOLALA)

1Thesalonike 4:16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

Hakika kuishi pamoja kunaleta furaha maishani. Kusudi la Mungu tangu kuimba dunia ilikuwa ni watu waishi pamoja tena kwa furaha daima wakimtukuza yeye (MUNGU). Lakini ni ale tu adui alipoingilia kati mpango huu mzuri na kuleta yaliyo kinyume. Dunia ikalaaniwa Mungu akatamka maneno makali na machungu kwa mwanadamu ikiwa tu ni matokeo ya kuiasi agizo lake la kutolila tunda mwanzo 2:17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika. Lakini ni pale tu Adam na Hawa walipodanganywa na shetani nao wakalila lile tunda tamko hili lilitimia.

Kwa mara ya kwanza ulimwengu unashuhudia huzuni unaoletwa na matokeo ya dhambi. mwanzo 4:8 Kaini akamwambia Habili nduguye, Twende uwandaniIkawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua. Wazazi wetu wa kwanza kabisa wanashuhudia kile Mungu alichowaambia kikitokea katika familia yao. na hivyo kumekuwa na misururu ya matukio ya vifo ambavyo kiuhalisia haviwezi kuelezeka katika lugha ya kueleweka. Matukio kama vile kujiua, kuuawa, ajali za moto majini nchi kavu, magonjwa njaa, majanga ya asili, vita na mengine mengi yamekuwa ni vyanzo vya vifo kwa wanadamu. Lakini ukweli ni kwamba kifo ni MPANGO WA SHETANI.

Ulimwengu wa leo kila kona ni vilio. Kifo ni kibaya, kifo hakitamaniki, kifo hakielezeki wapendwa, kifo hakizoeleki. Jamii inapoteza watu mashuhuri kwa sababu ya kifo, tunawapoteza wapendwa wetu kwa sababu ya kifo, tunapoteza watu tunaowategemea kwa sababu ya kifo, tunapoteza watoto, tunapoteza wenzi, tunapoteza wazazi, tunapoteza marafiki kwa sababu tu ya kifo. Hakika kifo ni mbaya. na kibaya zaidi ni kwamba tunapotengana nao hatuwaoni tena, wala hatuwasikii tena. Wanatuacha na huzuni, kilio, majonzi, shida, dhiki, taabu na mateso mengi, zaidi sana hutupelekea katika misongo ya mawazo na hata kutusabibishia sisi nasi kufa. Habari mbaya ni kwamba hata sisi tulio hai leo ni marehemu watarajiwa

Ni kwa sababu ya kifo hata leo jamii imetofautiana juu ya kile hasa wanachoamini kuhusu kifo. Wengi hudai kuwa mtu akifa ndio mwisho wake wa kuwepo duniani milele na milele (no life after death), dhana hii hudai kuwa mtu akifa anapelekwa pagatori huko ndiko anapokea hukumu yake kutoka kwa Mungu, kama alikuwa mdhambi basi hupokea mateso hukohuko na kama alkuwa mwenye haki basi roho yake huenda peponi kupumzika. Iko dhana nyingine inayoamini katika maisha baada ya kifo (there is life after death). Dhana hii hudai kuwa mtu anapokufa huyarudia mavumbi na husubiri siku ya kiama Bwana atakapokuja kuwachukua watakatifu wake nao waliokufa katika Bwana watafufuka kwanza.

Lakini ukweli hasa kuhusu habari ya wafu iko vipi katika Biblia??

Mwanzo 3:19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi. Bwana Mungu alipozungumza na Adam baada ya kula tunda alimwambia atayarudia mavumbi maana ndiko alikotoka. Ama hakika mtu anapokufa huyarudia mavumbi lakini naye hajui lolote muhubiri 9:5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. (soma pia Ayubu 14:21). Ni wazi kuwa mtu anapokufa huenda kaburini na hana mawasiliano tena kwa kuwa fahamu zake zimemtoka naye hufanana kama gogo lilikatwa likaangushwa huku likioza.

Habari njema ni kwamaba Bwana wetu Yesu Kristo aliushinda mauti naye ndiye anatupatia ahadi ya kuishinda mauti vilevile. Warumi 5:17 Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. Yeye Mungu mwenyewe aliyetamka kuwa tutakufa hakika ndiye pekee aliyeishinda mauti na kwa kupitia yeye nasi tutaishinda mauti. (1wakorintho 15:12-28)

Sasa basi ikiwa tutaamini kuwa hakuna maisha baada ya kifo tutakuwa upande wa wale wanaosema hakuna ufufuo nao siku ya kiama (kwa kuwa kama mtu akifa anapokea stahili yake pagatori na roho yake huenda peponi basi hakuna tena ufufuo) nao wanapingana na ukweli juu ya kufufuka kwake Kristo. 1 wakorintho 15:13,14 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka; tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.

Tunaambiwa ikiwa alifufuka basi nao wafu watafufuliwa……….. lakini kama tutaamini kuwa kuna maisha baada ya kifo tutaamini kuwa kuna ufufuo wa wafu nasi twaamini kuwa Kristo alifufuka katika wafu limbuko lao waliolala. 1wakorintho 15:20 Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Hii ni dhahiri kwamba fundisho juu ya kutokuwepo kwa ufufuo au kusema kuwa wafu huenda pagatori ni kinyume na biblia nayo hupingana na ukweli kuwa Kristo alifufuka.

1 wathesalonike 4:13-18 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo.

Mtume Paulo hakuacha kuzungumzia habari hii ya wafu kwakuwa mafundisho ya uongo kuhusu hali wafu yamekuwepo tangu zamani. Pualo anawaambia wathesalonike kupitia barua yake kuwa kwa habari ya wafu hakuna haja ya kusiskitika na kuishi bila tumaini kwa kuwa waliokufa katika Bwana watafufuliwa kwanza siku ya marejeo ya pili ya Kristo kuwachukua watakatifu wake. wapendwa ukweli ni kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na akafufuka ishara ya ushindi. Akatuachia tumaini la kufufuka siku ya mwisho. Swali kwangu na kwako je tunatumaini katika Kristo?? Je tunajiaandaje ikiwa tutakabiliwa na kifo leo tutakuwa tumeweka wapi tumaini letu?

Katika marejeo ya pili ya Kristo atawachukua walio watakatifu wake. kristo atakaporejea atakuta makundi manne ya watu. 1. Kundi la wenye haki walio hai, 2. Kundi la waovu walio hai, 3. kundi la wenye haki waliolala, 4. kundi la waovu waliolala. Angalizo” atakapotokea Kristo mawinguni na jeshi lake la malaika wakizipiga tarumbeta ‘wale wenye haki waliolala watafufuliwa kwanza, wao pamoja na wenye haki walio hai watavikwa miili ya kutokufa na kuondolewa miili ya kufa’. 1 wakorintho 15:52,53 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. hapo ndipo tutakapoungana kumlaki mwokozi hewani (1 wathesalonike 4:17). Wakati huo, wale waovu waliolala hawatafufuka (isipokuwa wale waliomchoma “ufunuo 1:7’ watakaofufuliwa kushuhudia utimilizo wa kile Kristo alichosema kisha walale tena) nao waovu walio hai watakufa wasioune utukufu wa Mungu kwa sababu ya dhambi zao wakikimbia na kuuambia milima iwasitiri (Ufunuo 6:16). Nao watadumu katika hali ya wafu kwa miaka 1000 huku watakatifu nao wakitawala na Bwana juu mbinguni kwa miaka 1000. Ufunuo 20:4

Wapendwa wangu, kifo si kitu kizuri, kifo hutuletea huzuni nyingi na vilio vikuu kila siku katika maisha yetu. Kifo hututenganisha na wapendwa wetu. Kifo hakibishi hodi, wala hakitoi taarifa. Leo uko hai, kesho unalala, leo tunasalimiana kesho hatusemeshani tena, kifo huja kwa wakati usiotegemewa. Hakuna hata mmoja aliyewahi kujua saa ya kufa kwake. Habari mbaya zaidi ni kwamba kifo hutuijia katika saa tusiyotarajia. Hutuijia katika saa tusiyojiweka tayari. hutuijia katika saa tusipokamilisha mipango yetu. Wengine hukutwa katika nyakati za furaha kabisa kifo huwachukua, wengine wakiwa na malengo makubwa kabisa kifo huwakatisha. Hakika tunateswa sana na kifo. Na tutakufa ni kweli.

Umejiandaaje kabla ya kufa?? Umejiweka tayari kiasi gani wakati huu ungali hai? Tumaini lako umeliweka wapi nyakati hizi una nafasi?? Nakupa shauri, WEKA TUMAINI LAKO KWA KRISTO. Fanya uhusiano mzuri na Kristo madam muda ni sasa. Utakapolala ulale katika tumaini la kumuona Bwana. Maana aliushinda mauti nasi tutaushinda mauti ndipo tutakapovikwa miili ya kutokufa na kuiluza mauti kuwapi kushinda kwako?? 1wakorintho 15:55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?... Tamanio langu ni kumuona Kristo ajapo mara ya pili, ikiwa ndio tamanio lako muombe Mungu leo akupatie ROHO MTAKATIFU akukumbushe kuzihesabu siku zako, uishi ukijiandaa muda wowote maana hatujui ni lini zamu yetu itafika.

BWANA AKUBARIKI

BY; PR. PETER I. JEFTER
0783167164
peterjefter91@gmail.com

Sunday, 21 May 2017

KILIO CHA USIKU WA MANANE



                                           KILIO CHA USIKU WA MANANE
                                                     (MIDNIGHT CRY)

Mathayo 25:6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.

Bila shaka tukizungumzia arusi hakuna yeyote anayeweza kuwa na swali juu ya namna arusi inavokuwa. Katika arusi kwa kawaida lazima kuwepo na Bwana arusi, Bibi harusi, wapambe vyakula nk. Kwahiyo sherehe inakuwa kubwa watu wanafurahi siku hiyo na hasa kwa anayeoa au anayeolewa na hata ndugu jamaa na marafiki. Kwa kweli furaha ya arusi ni ya pekee ambayo kila mtu maishani mwake hubaki kusimulia popote anapokuwepo.

Katika mafundisho ya Yesu kwa wanafunzi wake na hata makutano waliomzunguka alipenda sana kufundisha juu ya ufalme wa Mbinguni (ufalme wa Mungu kama inavyoweza kuzoeleka kwa wengine) na ndiyo maana aliwapa pia wanafunzi wake jukumu la kuhubiri juu yua ufalme wa Mbinguni. Mathayo 10: 7 Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.

Katika sura ya 25:1-13 ya kitabu cha mathayo Yesu anatumia kisa cha Arusi kutoa fundisho muhimu juu ya ufalme wa mbinguni na maandalizi ya wale wanaohusika katika arusi hiyo. Mathayo 25:1-5 Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. 2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. 3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; 4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. 5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi

Kisa hiki Yesu anakitoa maalum sio kutujengea mazingira ya kuelewa arusi inavyokuwa lakini kutupatia picha halisi juu ya ufalme wa mbinguni na marejeo yake kuwafuata walio wake. Katika kisa hiki kuna wanawali kumi wakiwa katika makundi mawili tofauti watano wakiwa ni wapumbavu na watano wakiwa wenye busara. Wengine waweza kudhani kuwa kisa hiki huzungumzia makundi mawili ya walio kanisani na walio nje ya kanisa LA!

Somo hili huzungumza juu ya watu wote waliomo ndani ya kanisa na halina uhusiano kabisa na walio nje ya kanisa kama ambavyo wengine wanaweza kudhani. Sababu zifuatazo huthibitisha kuwa wanawali hawa huwakilisha watu waliomo ndani ya kanisa. 1, wote ni wanawali maana kuwa wote wamejiandaa na tukio la Arusi (kurejea kwa mwokozi), 2. Wote wana taa lakini ni wenye busara tu ndio waliohifadhi mafuta wapumbavu hawakukumbuka kuhifadhi mafuta maana yake ni kuwa wote walipokea nuru lakini ni wachache walikubali kuitumia ile nuru waliopokea.

Kwa kufafanua zaidi makundi haya mawili tuanze kwa kuangalia kundi la wapumbavu. Kama ambavyo tumekwisha kuona kuwa wanawakilisha watu waliomo ndani ya kanisa waliopokea kweli ya Biblia lakini hawakuwa tayari kubadilishwa na ile kweli, maandalizi yao ya kumpokea bwana arusi (Yesu kristo) haukufanyika katika viwango vinavyopaswa. Pamoja na kuisikia sauti ya Mungu kila siku lakini hawakukubali kubadilisha maisha yao na kumfuata. Kila siku walisikia maonyo juu ya maovu yao lakini hawakuwa tayari kuacha, walisikia miito juu ya kufanya matengenezo katika maisha hayo lakini hawakujali. Walienda kanisani kama desturi lakini hawakuelewa maana halisi ya kwenda kanisani, na wakidai kujiandaa na marejeo ya pili ya Yesu kristo Ezekiel 33: 31 Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao. Soma pia mathayo 15:8

Kundi hili pia huonesha kuishiwa mafuta ya taa wakati wa kuwasili kwa Bwana arusi wakati wa siku wa manane humaanisha kuelemewa na maisha ya ulimwengu na yaliyomo hata kujisahau kuwa tayari kwa marejeo ya mwakozi. Wanawali wapumbavu walikuwa na mafuta kidogo kiasi cha kwamba isingeweza kustahimili hata wakati wa usiku wa manane anapokuja bwana arusi, maana yake ni kwamba wale walio ndani ya kanisa na wanauelewa mdogo wa kweli hataweza kustahimili dhoruba zitazowapata wale wanaomngojea kristo. Lakini pia hawa wanawali wapumbavu wanaonekana walitarajia marejeo ya bwana arusi kutokea mapema hali amechelewa hadi usiku wa manane, ndivyo ilvyo kwao hao walio ndani ya kanisa wakitarajia marejeo ya Yesu kuja upesi na wanapoona kristo anachelewa hulala usingizi wa kiroho na kujisahau kabisa kufanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kumpokea Kristo, hawa ndio wale walioingia harusini bila vazimaalum la arusi 

Kundi la pili katika kisa hiki ni kundi la wanawali watano wenye busara waliotunza mafuta yao hata alipokuja bwana arusi. Kundi hili huwakilisha kundi la wafuasi halisi wa kristo wale wanamatengenezo safi walioisikia sauti ya Mungu na kuruhusu mabadiliko ya kweli katika mioyo yao. 

Hawa ni wale ambao walipoisikia sauti ya Mungu hawakugeuza miguu yao kuzirudia njia zao mbaya za zamani. Mathayo 2: 12 Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine. Kutunza mafuta hata wakati wa usiku ni maandalizi mazuri ya kungojea marejeo ya pili ya mwokozi bila kujali ni lini atakuja. Hili ni kundi la wale waliompokea roho na kukubali kuongozwa nayo. Yohana 14:16,17 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

Mara ilipofika usiku wa manane ndipo kelele ziliposikika mathayo 25:6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. (And at midnight there was a cry made, Behold, the bridegroom cometh; go ye out to meet him .KJV). Biblia ya kingereza (toleo la king james) huzungumzia kile kinachozungumzwa katika biblia ya Kiswahili kama kelele kuwa ni kilio (cry), ambayo humaanisha kuwa wakati alipowasili Bwana arusi katika mji kulitokea kilio. Huenda watu hawa walilia kwa sababu hawakutarajia ujio wa Bwana arusi katika nyakati zile, yawezekana walishajisemea moyoni kuwa Bwana arusi amechelewa au ameghairi safari. ya arusi na hivyo watu wakalala. Ni hivyo kutokea kwa Bwana arusi katika wakati ule ulisababisha mshtukizo mkubwa kwa walio wengi.

Ndipo wanawali wote wakashtuka kwenda kumlaki Bwana arusi mathayo 25:7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao habari mbaya zaidi ni kwamba waliposhtuka wale wapumbavu walijikuta taa zao zikishindwa kuwaka. Kwa haraka njia walioona sahihi kwao ni kuomba mafuta hata kidogo kwa wale wenye hekima ili angalau taa zao zistahimili mikiki ya usiku ule. 

Kile kinachozungumzwa katika Biblia kama usiku wa manane ajapo bwana arusi humaanisha giza la kiroho, giza la kiroho lipo karibu kuifunika dunia kwa kuwa watu wameikataa kweli Amosi 8:11,12 Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana. Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la Bwana, wasilione. kutokuwepo kwa nuru tena kwa walio wengi. Watu watalala usingizi wa kiroho kwa kudhani kuwa mwokozi amechelewa kuja watu watajisahaulisha kuendelea kutafuta ukweli wa biblia. Kama ilivyokuwa katika kipindi cha nuhu ndivyo itakavyokuwa kipindi hiki ajapo mwokozi wa ulimwengu. luka 17:26, 27 Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu. Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote. Kama ilivyokuwa katika siku ya gharika watu walipomkimbilia nuhu wakihitaji wafunguliwe waingie kuepuka kifo cha milele lakini Nuhu hakuwa na uwezo wa kufungua safina ndivyo walivyokimbia wanawali wapumbavu wakihitaji msaada wa mafuta na wo wanawali wenye hekima hawakuweza kuwapatia mafuta, ndivyo itakavyokuwa kwetu pia, vile tutapuuzia kujiandaa kwa ajili ya siku ya ujio wa Bwana hatutaweza kupata msaada wowote toka kwa mtu yeyote yule. Ni fundisho kwetu kuwa maandalizi ya mtu mwingine hayataweza kumwokoa mtu mwingine na imani ya mtu haiwezi kuokoa imani ya mwingine, hivyo imetupasa kujiandaa maadam kungali bado mchana

Wakati ambapo watu watakuwa wamejisahau kuutafuta ukweli wa Mungu, wakati ambapo ulimwengu utakuwa umekuwa busy kwa shughuli za maendeleo, wakati wakazi wa ulimwengu wakifurahisha kwa anasa na kila aina ya starehe za kidunia ndipo atakapokuja mwana wa adamu. 1 wathesalonike 5:3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. Hakuna binadamu awaye yote atakayeweza kuokolewa kwa maandalizi hafifu. Yatupasa kujiandaa kungali mapema na tujiweke tayari kwa ujio wa mwokozi.

Matahyo 24:42-44 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja. Ni fundisho kwetu kuwa tusikadirie muda wa marejeo ya mwokozi na hapo tuonapo kuchelewa tunakata tama, imetupasa kujiandaa kila iitwapo leo kumlaki mwokozi maana saa yaja hatoweza mtu kufanya maandalizi yoyote. Imetupasa kukesha kwa maombi. 1 wathesalonike 5:17 ombeni bila kukoma. Kwa maana hatuijui siku wala saa atakapokuja. Na atakapokuja tusijekuwa kama wale wanawali wapumbavu

BWANA AWABARIKI

BY; PETER I. JEFTER
0783167164
peterjefter91@gmail.com

UNAFANYA NINI USIKU WA MANANE



UNAFANYA NINI USIKU WA MANANE??

Matendo 16:25 Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.

Unaposikia neno usiku wa manane unaelewa nini???

Kwa tafsiri rahisi usiku wa manane ni masaa ya usiku yaanzayo saa 6 hadi 8 au 9 ndiyo kwa lugha rahisi hujulikana kama usiku wa maneno. Kwa kawaida masaa haya ni masaa ya pekee sana katika historia ya siku. Katika sehemu nyingi duniani masaa ya usiku wa manane ni masaa ambayo kwayo watu wote wamelala ikiwa ni vijijini kijiji kizima kinakuwa kimya masaa haya maana shughuli zote zimesimama. Kwa maeneo ya mjini masaa haya pia dunia huwa kimya na hata kama kuna shughuli za kimaendeleo zinafanyika basi ni chache sana na huenda kwa sehemu chache pia.

Usiku wa manane ni masaa ambayo kwa asilimia kubwa dunia inakuwa imetulia kimya maana shughulu nyingi zimesimama, usiku wa manane ni masaa ambayo kuna giza nene pasipo mwanga hata mdogo huwezi kutembea hata hatua moja. usiku wa manane ni nyakati ambazo kwazo shughuli nyingi za kiualifu hufanyika maana watu wanakuwa wamelala wasijue chochote kinachoendelea huko nje. Usiku wa manane ni masaa ambayo mtu haoni mbele nyuma wala pembeni kwa kuwa kote kumetanda giza na hakuna mwanga. Ni nyakati ambazo hata ukikutana na mtu kumwamini inakuwa shida maana hujui kusudi lake katika nyakati hizo ni nini zaidi sana utamdhania kuwa si mtu mwema.

Usiku wa manane unafanya nini????

Kisa cha Paulo na Sila kinaanza katika matendo ya mitume sura ya 15 wakiwa Antiokia matendo 14:26 Na kutoka huko wakaabiri kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza. katika shughuli zao za uinjilisti mara baada ya Paulo kuongoka.katika sura ya 15:1 Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka. Kwa sababu ya mjadala wa kidini juu ya kutahiriwa au kutokutahiriwa kwa wale wamataifa walioongoka wapya kama torati ya Musa ilivyoamuru walishindwa kufikia muafaka kwa sababu wapo walisema ni lazima kutahiriwa na waliosema si lazima kutahiriwa.

Kwa sababu ya mabishano hayo Paulo na Barnaba waliamua kupanda kwenda Yerusalemu kuwauliza wazee wa baraza na baadhi ya mitume waliokuwepo hapo akiwemo na Petro Matendo ya mitume 15:2 Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo. Baada ya mahojiano katika baraza na Petro kutoa hitimisho (matendo 15:7-11) Paulo na Barnaba wanarejea Antiokia na uhjumbe waliopewa. Na ndipo walipohitaji kurejea katika hiyo miji waliowahi kupeleka injili ili kuwajulia hali hao waongofu. Barnaba anamchukua marko (yohana), na Paulo anamchukua Sila (fungu la 36-41)

Wakipita katika miji kama Derbe, Listra, ikonio, firgia na Galatia kote huku walikuwa wakihubiri habari njema wakapita Misia wakatokea Troa. (Matendo 16:1-8). Ndipo Paulo anazuiliwa na Malaika asihubiri katika Asia lakini matendo 16:8 Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia. Ndipo

Fungu la 8 Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. Hata ilipofika sabato walitafuta kanisa ili wasali matendo ya mitume 16:13 Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. Mmojawapo wa wanawake hao alikuwepo mwanamke aliyeitwa Lidia.

Tukio la ajabu na la pekee linaliokumba safari ya Paulo na sila huku Makedonia ni kukutana na binti kijakazi aliyekuwa na pepo wa uaguzi aliyewapatia bwana zake faida kwa kuagua matendo ya mitume 16:16 Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. (kuagua ni nini??) paulo alisikitishwa sana na kitendo cha yule binti kupiga kelele mara kwa mara na hivyo alimuamuru yule pepo kumtoka yule binti nayo pepo ikamtoka saa ile ile matendo ya mitume 16:18 Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.

Binti huyu alikuwa ni chanzo zha mapato kwa bwana zake maana kwa kitendo cha uaguzi aliwapatia faida. Kitendo cha Paulo kumtoa pepo kilizua tafrani maana bwana zake waliona sasa wamepoteza chanzo cha mapato. Waliwakamata Paulo na Sila na kuwapeleka sokoni mbele za wakuu wa mji matendo ya mitume 16:19 Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji; usicheze na chanzo cha mapato cha mtu hasa wakubwa!! waliadhibiwa na kuchapwa kwa bakora na kasha kuamriwa kutupwa gerezani na kufungwa na mkatale matendo ya mitume 16:23,24 Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. (mkatale ni ubao uliotobolewa unaingizwa miguuni na kufungwa kwa kufuli)

Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwimba Bwana na kumwimbia nyimbo za kumsifu na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Matendo ya mitume 16:25 Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Katika hali isiyo ya kawaida si rahisi kuwakuta mahabusu au hata wafungwa wakiwa ndani ya cello (korokoroni, kifungoni) wakifanya hata ibada, mara nyingi wengi wakishafika kule hupoteza tumaini na kuona kama ndio mwisho wa maisha yao hata kama ulipelekwa kwa kusingiziwa ama kuonewa. Na ukifika katika gereza huwezi kusikia hata sauti ya mtu ikiimba nyimbo za Kristo zaidi sana ataimba nyimbo za kiduni (jela ni mbaya jela ni amteso). Lakini hapa tunakutana na wafungwa wawili jasiri ambao pamoja na kupigwa kwingi na kufungwa na mikatale bado hawakujali maumivu wala uchovu waliokuwa nao (maana huenda kwa sababu ya maumivu ya viboko na mkatale wangeamua kulala zao wakisubiri adhabu ambayo ingewakabili kesho yake) lakini watu hawa wanamuomba Mungu na kumuimbia nyimbo za kumtukuza

Matokeo ya maombi na nyimbo hizi ni tetemeko kubwa katika nchi yote na misingi ya gereza ikatikisika vifungo vyote vikalegea matendo ya mitume 16:26 Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa. Ni kwa nguvu ya maombi na nyimbo milango ya gereza ikafunguka mlinzi aliogopa hata kutaka kujiua lakini paulo alimsihi asijiue maana hawajatoroka lakini kubwa zaidi waliamuriwa watolewe gerezani maana wakuu wa mji waliogopa kwa tukio lile.

unafanya nini usiku wa manane??
Usiku wa manane kwako ni nini? Ni changamoto gani unayoipitia katika maisha yako? Ni jambo gani kubwa kwako linalokuzinga hata usimuone Kristo sasa? Giza lipi limekufunga hata huoni nuru tena, ukiangalia mbele ni giza nyuma giza pembeni giza? Tumaini lako liko wapi wakati wa giza nene lililokuzingira pande zote?

Huenda usiku wa manane kwako ni ugonjwa, umeugua kwa muda mrefu sasa na huoni tena tumaini katika maisha yako ukidhani ndio mwisho wako… huenda usiku wa manane kwako ni changamoto za ndoa au mahusiano ya uchumba na sasa unalia kila siku huoni tumaini tena, huenda usiku wa manane kwako ni ajira na shughuli zako za kiuchumi zinazokuwia ugumu kila siku na sasa unapoteza tumaini… huenda usiku wa manane kwako ni changamoto ya kiimani unayoipitia katikati ya ndugu zako jamaa au hata rafiki, unafukuzwa kazi kila siku kwa sababu ya imani nawe huoni tena tumaini… umefungwa na nini? Paulo na sila walifungwa na mkatale……

Kumbuka ni katika usiku wa manane imetupasa kumuita Kristo kuliko nyakati zote tumewahi kumuita. Ni katika usiku wa manane imetupasa kumuomba Mungu na kumuimbia nyimbo za sifa hata wafungwa wengine wasikie.. ni kwa maombi na nyimbo tetemeko kuu litasikika katika nchi navyo vyanzo vya usiku wa manane kwako vitaogopa. Kama ni ndugu jamaa marafiki au waajiri wako wataogopa na kukupa uhuru wako, kama ni njaa misiba vita nk nk vitakimbia maana Bwana atajifunua kwako sasa. Maombi na nyimbo hutikisa misingi ya muovu

USIKU WA MANANE OMBA NA KUMUIMBIA MUNGU NYIMBO ZA SIFA

BWANA AWABARIKI


BY Pierre de' Jefter
0783167164
peterjefter91@gmail.com

Friday, 19 May 2017

MTU WA NNE KATIKATI YA MOTO



MTU WA NNE KATIKATI YA MOTO
(The forth man in the midst of fire)

Daniel 3:25 Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.

Bila shaka katika maisha ya kawaida imeozoeleka kuwa kila jamii huwa na desturi au tamaduni zake, na hivyo tamaduni hizo hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine. Kwa mfano tamaduni za kiafrika kwa sehemu kubwa hutofautiana na tamaduni za wazungu au waarabu wachina nk. Mambo haya ya kutofautiana kwa tamaduni hayakuanza leo lakini ni tangu miaka na miaka na hata katika habari za ibada pia kutofautiana kwa tamaduni kupo. Wakati wengine wakimwabudu Mungu wa kweli wengine wanaabudu Miungu mingine, wengine hutofautiana katika kubatiza wengine kufundisha biblia wengine hata siku za kuabudu.

Mpendwa msomaji naomba nikuulize swali, hebu fikiria katika tamaduni yako uliyoizoea labda iwe ni tamaduni ya kijamii au ya kiroho alafu ukaenda katika jamii nyingine ukakuta tamaduni nyingine tofauti kabisa na yako, hali ukijua ni mbaya na haifai kwako lakini sheria za jamii ile inakulazimisha kuacha tamaduni yako na kufuata ya kwao vinginevyo ukutane na adhabu kali amabyo huenda ni ya kifo, utafanyaje???????

Hali kama hii ndiyo inayowakuta vijana watatu wa kiebrania waliochukuliwa utumwani Babeli. Mara baada ya kufika Babeli vijana hawa walitakiwa kuacha kabisa desturi zao za kiebrania na kufuata desturi za wakaldayo (Babeli). Na hivyo jaribu la kwanza lilikuwa ni kuwabadilisha majina ili wawe na majina ya kibabeli Daniel 1:7 Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita Danieli, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego. Kama hilo halikutosha walipaswa hata kula chakula cha wakaldayo Daniel 1:5 Huyo mfalme akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme. Lakini katika hili la chakula hawakuwa tayari kujitia unajisi kwayo hivyo waliazimu kutokula na zaidi wakapewa chakula kama kile walichozoea

Vijana hawa walionekana kuwa na maarifa na hekima zaidi sana walikuwa pia ni wazuri wa sura Daniel 1:4,6vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao. Basi katika hao walikuwapo baadhi ya wana wa Yuda, Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria. Na hio kwa sababu ya mafanikio haya wakaldayo hawakuwa na furaha juu yao wakakusudia kuwaangamiza. 

Na sasa walitakiwa kuacha tamaduni yao ya kumwabudu Mungu wao wa kweli na kuabudu Miungu ya wakaldayo. Katika tamadani ya wakaldayo waliabudu Miungu kama vile sanamu nk. Mfalme Nebukadneza anaamuru sanamu itengenezwe kubwa Daniel 3:1 Nebukadreza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli. Na akaamuru watu wote waletwe wasujudie sanamu ile. Ama lah! Atakayekataa kuisujudia sanamu ile atatupwa katika tanuru la moto mara moja.Daniel 3:6 Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao.

Kiashiria tu kiliposikika kila mtu alipaswa kuanguka na kusujudia sanamu ile Daniel 3:5 wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. Katika hali isiyoweza kuelezeka hili lilikuwa ni jaribu kuu na kubwa kwa vijana waebrania ambao sasa wanalazimishwa kumuasi Mungu wao lakini ashukuriwe Mungu vijana hawa hawakuwa tayari kufanya hivyo. Ndipo kila aina ya ngoma iliposikika wakaldayo wote walianguka na kuisujudia sanamu ile isipokuwa wale vijana watatu tu wa kiebrania. Daniel 3:12 Wako Wayahudi kadha wa kadha uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki, na Abednego; watu hawa, Ee mfalme, hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako, wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. Vijana hawa walitambua ya kuwa kusujudu na kuabudu ni tendo la heshima kwa Mungu wa mbinguni pekee yake na hivyo kusujudia sanamu ilikuwa ni kuasi juu ya sheria ya Mungu mathayo 4:10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Soma pia (kutoka 20:4, 5)

Kutokana na kitendo hicho hakika ghadhabu ya mfalme ilipanda hata kuwauliza vijana kama huenda ni kwa makusudi walikataa kutii amri ya mfalme, ndipo mfalme Nebukadneza kwa ujinga wake akadhani kwa kuwapa nafasi ya pili wangethubutu hata kuinamisha vichwa Daniel 3:15 Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu? Vijana hawa kwa kutambua ukuu wa Mungu kwao hawakuwa na sababu ya kusujudia sanamu ya mfalme walichomwambia mfalme ni Daniel 3:16-18Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. Bila shaka vijana hawakuona haja ya kusujudia sanamu ile.

Kwa sababu hasira ya mfalme ilikuwa kali sana juu ya vijana wale aliamuru moto uongezwe mara saba na kuamuru vijana wale watupwe ndni ya lile tanuru la moto hali wamefungwa Daniel 3:19, 20 Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto. Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. Na kwa sababu ya ukali wa moto huu waliokufa wa kwanza walikuwa ni wanajeshi wa Nebukadneza waliomuriwa kuwatupa vijana wale ndani ya moto.

AJABU KULIKO AJABU ZOTE DUNIANI, Vijana hawa walitupwa ndani ya tanuru wakiwa watatu hali wamefungwa lakini sasa mfalme anaona wakiwa wanne hali wamefunguliwa na hawajadhurika hata kidogo. Tendo hili lilimtoa mfalme akili kidogo hata kushindwa kuelewa kama ni ya kweli anayoyaona au huenda anaota ikabidi atafute ushahidi kwa waliokuwa karibu naye huenda nao walikuwa wanaona. Lakini ndivyo ilivyokuwa wala Daniel 3:24, 25 Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme. Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu. Jambo linalomshangaza mfalme ni kuwa walitupwa watatu na sasa anawaona wanne tena yule wanne ana sura ya mwana wa Mungu. Kumbe hata mfalme alimtambua mwana wa Mungu JINA LA BWANA LITUKUZWE.

Ndipo mfalme akaamuru vijana wale watolewe ndani ya tanuru na kutoa agizo kwa kila mtu kumuabudu Mungu wa shadrack Meshack Shadrack na Abednego Daniel 3:28 Nebukadreza akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe.kisha mfalme akawatukuza vijana wale (fungu la 30)

Mpendwa rafiki je umeogopa kwa ajili ya moto uliowashwa kwa ajili yako??? Nakukumbusha kuwa yupo mtu wanne ataonekana katika tanuru la moto lililowashwa kwa ajili yako. Yohana 16:33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. Huenda ni kwa sababu ya mafanikio yako moto utawashwa kwa ajili yako ili ushushwe, huenda ni kwa sababu ya mali, utajiri, uwezo, au hata uzuri majaribu yatakuijia yenye ukali kama wa moto wa Nebukadneza usiogope maana mtu wanne ataonekana. Huenda ni kwa sababu ya imani yako matahayo 10:17-19 Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa. Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.

hata sasa jaribu la kuabudu sanamu ya mnyama iko mbele yetu nalo litatolewa tangazo kama lile la mfalme Nebukadneza. Ufunuo 13:15 Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Haya yote yajapotupata hatuna haja ya kuogopa kwa maana mtu wanne yupo nasi tukawe na jibu kama lile la kina shadrack, Meshack na Abednego Daniel 3:16-18Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.
NAWATAKIENI BARAKA ZA BWANA

WENU MJOLI WA BABA
PETER I.JEFTER
0783167164
peterjefter91@gmail.com/pierredejr2000@gmail.com

CHUKIZO LA UHARIBIFU



Chukizo la uharibifu
(The abomination of desolation)

Mathayo 24:15, Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Daniel, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu).

Sura ya 24 ya kitabu cha mathayo (mathayo 24) ni sura maarufu na maalum kwa matukio au dalili (ishara) za kurudi kwa Kristo. Yesu akiwa na wanafunzi wake akiwafundisha kuhusu ishara za marejeo yake hakuwaficha pia juu ya chukizo la uharibifu.

Lakini je chukizo la uharibifu ni nini??
Katika kipindi cha wana wa Israeli zamani hizo kitu chochote kilichokuwa kinyume na sheria za wayahudi au kilikuwa tofauti na ibada zao kilikuwa ni chukizo kwao. Kwa mfano kushikamana na wamataifa (wasiotahiriwa) ilikuwa ni chukizo kwa kuwa waliku najisi.

Tangu Misri Bwana hakuruhusu huduma zake takatifu zifanyike huko kwakuwa wamisri waliabudu Miungu mingine. Huduma zozote za kiibada zilizofanywa kinyume na ibada takatifu yalikuwa ni machukizo. Kutoka 8:26, Musa akasema, Haitupasi kufanya hivyo; kwakuwa tutamchinjia sadaka BWANA, Mungu wetu na hayo machukizo ya Wamisri; Je! Tutachinja sadaka ya hayo machukizo ya Wamisri mbele ya macho yao, wasitupige kwa mawe. Soma pia mwanzo 42:32 na 46:34. Wamisri na Waebrania kuchangamana ilikuwa ni machukizo.

Katika kipindi cha utawala wa Sulemani je? Kitendo cha Sulemani kuoa wanawake wengi pia kilikuwa ni machukizo kwa MUNGU 1Wafalme 11:5- 7 Kwakuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, Mungu mke wa wasidoni na Milkomu, chukizo la waamoni Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, wala hakumfuata BWANA kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. Sulemani akamjengea Komeshi, chukizo la wamoabu, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu na Moleki, chukizo la wana wa Amon. Soma pia 2Wafalme 23:13

Baada ya kuona maana ya chukizo. Turejee katika fungu letu la mathayo 24:15. Chukizo la uharibifu lililonenwa na nabii Daniel ni nini?? Na nini ishara zake?
Daniel 9:27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka ya dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo hata ukomo, na gadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
Mafungu haya ni muendelezo wa mafungu ya nyuma yakizungumzia juu ya unabii wa majuma 70 yaliyotabiriwa juu ya wayahudi na huduma ya YESU na kukataliwa kwa injili ndani ya uyahudi kisha kutoa nafasi kwa wamataifa kusikia injili.

Katika tafsiri ya majuma 70 tumeona ilianza mwaka wa 457 K.K na kuishia mwaka wa 34 A.D. juma moja la mwisho 
ambalo Yesu anaweka agano thabiti na watu wengi huanzia mwaka wa 27 A.D ambapo YESU alianza huduma yake duniani nayo huishia mwaka wa 34 A.D kukataliwa kwa injili na kuuawa kwa Stephano (matendo 7:54-60) ambapo nusu ya juma hilo. (kwakuwa juma lina siku 7 nusu yake itakuwa ni 31/2) huanza mwaka wa 27 A.D Kristo anapoanza huduma yake hadi 301/2 A.D anapokatiliwa na kuuawa. Nayo nusu nyingine huanza 301/2 A.D injili kwa wayahudi kwanza hadi 34 A.D wanaikataa injili na kuwaua watumishi wa MUNGU kisha mlango wa injili kwa wamataifa inafunguliwa.

Baada ya hayo ndipo litakaposimama chukizo la uharibifu, hii humaaisha kuwa baada ya huduma ya Yesu kukataliwa nao wayahudi pia kuikataa injili badala yake litasimama uharibifu mkubwa na machukizo mengi. Daniel 11:31 na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu hapa Biblia hutuambia juu ya pembe ndogo iliyoinuka katika (Daniel 8:9.) ambayo katika Daniel 8:11 Naam ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa. (patakatifu palipoangushwa hapa ni hekalu la Yerusalemu liliangushwa na utawala wa kirumi katika mwaka wa 70 A.D Luka 21:20 Lakini hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. Yesu alitabiri juu ya anguko la Yerusalemu katika Mathayo 24:2....... Amin nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa

Daniel 12:11 Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itakapoondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na sitini. (siku elfu mia mbili na sitini sawa na miaka 1260 huanza 538-1798 kuinuka kwa upapa hadi kutiwa kwake jeraha la mauti, Dan 7:25, ufunuo 13:3). Yesu anazungumzia anguko la mji wa Yerusalemu kama chukizo la uharibifu. Luka 21:20 Lakini hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. Kubomolewa kwa hekalu la Yerusalemu mnamo mwaka 70A.D huashiria mwisho wa taifa la Israeli na ambapo wengi wao walikimbilia katika mataifa mengine, wengine walichukuliwa mateka. Baada ya kipindi hicho ndipo ukainuka utawala wa upapa ulioleta mafundisho ya uongo na kutengua sheria za MUNGU na kulazimisha watu kuyashika yaliyo kinyume na kweli nacho kilikuwa kipindi kilichoitwa zama za giza ambacho kilidumu kwa miaka 1260..........

Chukizo la uharibifu unafananishwa na kipindi kinachokuja mbele yetu, atakaposimama Yule mharibifu mpinga Kristo. 2wathesalonike 2:1-4 Basi ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitishwe, kwa roho wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo, Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu, akafunuliwa kwanza YULE MTU WA KUASI, MWANA WA UHARIBIFU...........akijionesha nafsi yake ya kwamba yeye ni Mungu. Atakapo simama Yule mpinga kristo na kuhalallisha mafundisho ya uongo (angalia fungu la 9), pale sabato bandia itakapochukua nafasi ya Sabato halisi (jumapili kuchukua nafasi ya jumamosi) haya yote yatakuwa ni machukizo mbele za Mungu.
Ahadi ya MUNGU kwako.
Ufunuo 3:10 kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi name nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwenguwote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.

BWANA AKUBARIKI.


PETER I. JEFTER
0783167164
pierredejr2000@gmail.com

TUMAINI KATIKATI YA MAOMBOLEZO



TUMAINI KATIKATI YA MAOMBOLEZO


Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Kijana mmoja (John) anasimulia hivi; ilikuwa ni mwaka 2008 march ndiyo uliyokuwa mwisho wake kumuona Baba yake mzazi, akiwa ameishi na Baba yake kwa takribani miaka 17 ghafla siku moja akiwa shule alipokea taarifa za msiba wa Baba yake mzazi. Kijana huyu anasema aliposikia habari zile alishindwa kuamini kama ni kweli au si kweli. Ilimchukua zaidi ya nusu saa kurudia hali yake ya kawaida ili kuendelea kutafuta ukweli wa jambo lile. Lakini ilikuwa ni kweli mzazi wa kijana huyu alikuwa amefariki siku ile.

Kutokana na taarifa zile kijana huyu aliona kama naye muda wake wa kuishi duniani umefikia ukomo, kwani hakuona tena tumaini mbeleni kwa sababu mzazi wake huyu ndiye aliyekuwa kila kitu kwake kwani mama yake alishafariki miaka minne nyuma (2004), John alijua amepoteza kila kitu na hata elimu yake aliyokuwa akitafuta ilikuwa imefika mwisho. Mnamo siku ya mazishi ya Baba yake kijana John alipoteza fahamu kutokana na kilio kilichojaa uchungu kwa kuwa alipoteza tumaini ya siku za usoni. Mara ghafla sauti ya shangazi yake ilisikika masikioni mwake ikimbembeleza na kumsihi anyamae (nyamaza John usilie sana, nyamaza tu kama ni shule bado utaendelea na usihofu sana tutakusaidia, sauti ya shangazi). Hii ndiyo iliyokuwa sauti iliyoleta tumaini kwa kijana peter kwakuwa aliona yupo mfariji kwake ……………

Sura ya 29 ya kitabu cha Yeremia ni barua ambayo MUNGU anamuongoza yeremia kuandika na kuituma kwa watu walio uhamishoni (Babeli) ukiwa umejaa ujumbe wa matumaini. Yeremia 29:1 Maneno haya ndiyo maneno ya waraka, ambao nabii Yeremia aliupeleka toka Yerusalemu, kwa hao waliobaki wa wakuu waliochukuliwa mateka, na kwa makuhani, na kwa manabii, na kwa watu wote, ambao Nebukadreza aliwachukua mateka toka Yerusalemu hata Babeli; ieleweke kuwa wakati wana wa Israeli wakichukuliwa utumwani Yeremia alibaki Yerusalemu

Wana wa Israeli kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao na uasi wao na viongozi wao dhidi ya sheria ya Mungu, Mungu aliamuru watiwe mikononi mwa wafalme wa mataifa walioitawala dunia kwa wakati huo (Nebuchadnezzar mfalme wa Babeli) Yeremia 25:8,9 Basi Bwana wa majeshi asema hivi, Kwa kuwa hamkuyasikiliza maneno yangu, angalieni, nitapeleka watu na kuzitwaa jamaa zote za upande wa kaskazini, asema Bwana, nami nitatuma ujumbe kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitawaleta juu ya nchi hii, na juu yao wakaao ndani yake, na juu ya mataifa haya yote yaliyopo pande zote; nami nitawaangamiza kabisa, na kuwafanya kitu cha kushangaza, na kitu cha kuzomewa, na ukiwa wa daima.

Na hivyo iliwapasa kukaa utumwani kwa miaka 70. Yeremia 25:12 Na itakuwa miaka hiyo sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na taifa lile, asema Bwana, kwa sababu ya uovu wao, nayo nchi ya Wakaldayo pia; nami nitaifanya kuwa ukiwa wa milele. Ujumbe wa sura ya 29 unapotumwa ndipo tu miaka 10 ilikuwa imepita kwahiyo vijana bado walikuwa na safari ya miaka 60 kuendelea kukaa utumwani (kwa msaada kwako msomaji wana wa Israeli walipelekwa Babeli kwa mara ya kwanza mwaka 605 K.K na ilipofika mwaka 539 K.K ndipo ulipofika mwisho wake). 

Katika kipindi hiki kigumu ambacho watu hawa wa Mungu waliomuasi wanapitia nyakati ngumu za utumwa (fikiria hali ya kufanywa kuwa mtumwa katika nchi ya ugeni, taifa lililokuwa likiongozwa na kiongozi dictator na katili ajabu Nebukadneza), bila shaka wana wa Israeli walipoteza matumaini kabisa na huenda hawakuona tena ukombozi mbele yao hasa katika taifa la kijeshi lililotawala dunia nzima.

Makosa yaliyofanywa na viongozi na wana wa Israeli yalikuwa ni kukataa maonyo ya Mungu yaliyoletwa kwao kupitia kwa watumishi wa Mungu, kumbuka hata safari ya Israeli kutoka Misri kwenda Kaanan mioyo yao ilikuwa migumu hakika. Katika kipindi hiki Mungu anamtumia nabii wake Yeremia kupeleka maonyo kwa viongozi na raia lakini hakuna hata aliyeonekana kujali. Si kiongozi wala si mwananchi aliyeonekana kusikiza kile Mungu alichonena kupitia kwa nabii Yeremia 

Pamoja na uasi mkuu wa namna hiyo, pamoja na kukaa utumwani kwa muda wote huo lakini bado BWANA hakuwasahau watu hawa. UPENDO MKUU ULIOJE!! . ujumbe wa matumaini unatumwa kwa watu waliopoteza tumaini. Bila shaka watu hawa walikuwa katika hali ya masikitiko na maombolezo mengi kwa sababu ya mateso, dhiki na manyanyaso mengi waliyokuwa wakiyapitia katika nchi ya ugeni. Huenda hawakujua ni wapi wokovu wao ungepatikana hasa ukiangalia aliyekuwa kiongozi wao kwa wakati huo (Yehoyakini) alifanywa mateka pamoja na familia yake na walielewa wazi ya kuwa huenda Mungu asingewaletea

ukombozi tena kwa kuwa walishayaacha maagizo yake na hivyo walijua hakika Mungu amewaacha.
Habari pekee inayoleta matumaini kwa watumwa hawa (wana wa Israeli) inatoka kwa yule yule aliyeruhusu waende utumwani, naye ni Mungu pekee. Hili hutufundisha upendo mkuu wa ajabu na usioelezeka alionao Mungu kwa watu wake hata wajapomuasi kwa kiasi gani.Yeremia 29:10 Maana Bwana asema hivi, Babeli utakapotimiziwa miaka sabini, nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno langu jema kwenu, kwa kuwarudisha mahali hapa. Mungu alitaka wana wa Israeli watambue ukuu wake lakini bado mioyo yao ilikuwa migumu. Bwana akaamua kuwaadhibu kupitia kwa utawala wa kidunia. Hivyo iliwapasa kukaa utumwani kwa muda wa miaka 70 ndipo wokovu utakapowajia.

Ndipo Mungu huyu huyu waliyemkataa na kumuasi anawapa ujumbe uliojaa tumaini ujumbe unaoleta faraja katika nyakati za za maombolezo na huzuni nyingi. Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. Hii ilikuwa ni habari njema kwa watumwa hawa waliomkataa Bwana wao. Kumbe siku zote za matukio makubwa kama hayo bado Bwana aliwawazia mawazo ya amani wala si ya mabaya lakini zaidi sana kuwapa tumaini katika siku za mwisho. Mipango ya Mungu juu ya wokovu wa wana wa Israeli toka utumwani bado ulikuwepo lakini safari hii ilikuwa ni mpaka zitimie miaka 70.

Pamoja na maovu yote ambayo wana wa Israeli walitenda, pamoja na uasi wote ambao wana wa Israeli walifanya dhidi ya maonyo ya Bwana lakini bado Rehema za Bwana zilikuwa juu yao, neema na upendo mwingi wa Bwana bado ulikuwa pamoja nao. Na hivyo iliwapasa wana wa Israel kumtafuta Bwana na kumrudia Yeremia 29:12-14 Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. Nami nitaonekana kwenu, asema Bwana, nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa, nami nitawakusanya ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote, na katika mahali pote, nilikowafukuza, asema Bwana; nami nitawaleta tena, hata mahali ambapo kutoka hapo naliwafanya mchukuliwe mateka. Iliwapasa wana wa Israeli kuutafuta uso wa Mungu hata katika nyakati ngumu za namna gani walizokuwa wakipitia.

Wengi wetu leo tupo katika utumwa mzito tena mgumu wa dhambi, haya yote ni matokeo ya kukataa kusikia na kutii sauti ya Mungu. Kama ilivyokuwa katika siku za wana wa Israeli. Mungu ameruhusu tupitie katika vifungo hivyo vya utumwa kwa sababu ya kukataa kutii maagizo yake leo. Mathayo 15:8, 9 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.

Kama ilivyokuwa kwa wana wa Israeli ndivyo ambavyo imekuwa hata leo. Sauti ya Mungu tumeisikia lakini hatujataka kuenenda kama inavyotuagiza. Wengu wetu tupo katika utumwa wa dhambi, dhambi za uongo, ulevi, uasherati, wizi, masengenyo, kuabudu sanamu, uzinzi na kila aina ya dhambi wengine wanapitia hali ngumu za maisha njaa, magonjwa, misiba nk. Pamoja na hayo yote bado ujumbe ule ule wa matumaini uliotoka kwa Mungu kwenda kwa wana wa Israeli waliokuwa utumwani ujumbe wa amani na matumaini bado unakuja kwetu hata leo. Bwana hajatuacha kwa sababu ya hali zetu za dhambi, Bwana hajatuacha wapendwa kwa sababu ya kutanga mbali naye bado anatuita leo tumrudie naye atatufanya kuwa wapya. Huenda miaka yako 70 ya utumwa wa dhambi ya uzinzi ni leo, huenda huu ndio muda wako wa kuokolewa. Mathayo 11:28, 29 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; huu ndio wito wa Bwana kwetu leo, yeye Mungu anayetuwazia mawazo ya amani anatuita twende tusemezane 

Isaya 1:18, 19 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; Upendo, neema na Rehema za Mungu bado zipo nasi hata leo imetupasa kumtafuta Bwana maadam anapatikana. Isaya 55:6,7 Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.

Rehema za Mungu zipo kwa kila amtafutaye, tazama saa ya wakovu kwako ndiyo sasa saa iliyokubalika ndiyo hii. 2wakorintho 6:2 Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa) Mrudie Bwana maana yupo tayari anakungoja. (Ufunuo 3:20, 21)

BWANA AWABARIKI.

Peter Jefter
0783167164
pierredejr2000@gmail.com





SIMAMA TAZAMA KALVARI

SIMAMA TAZAMA KALVARI

1Wakorintho 1:18 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

Matokeo ya dhambi yalipelekea kusudi zima la Mungu kuumba dunia kutoweka. Hapo awali Mungu aliumba dunia katika uzuri na ukamilifu wake na kila alichofanya Mungu kilikuwa ni chema Mwanzo 1:31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita. Na hivyo mpango wa Mungu ulikuwa ni kufanya kila kitu kiwe chema na duniani pawe mahali pema kwa binadamu na viumbe vingine vyote alivyoviumba Mungu.

Mara tu baada ya anguko la mwanadamu dhambini kila kitu kilibadilika na uso wa dunia uligubikwa na huzuni kwa kuwa muasi ameleta badiliko hasi tofauti na kile Mungu alichokusudia. Dunia iliyoumbwa na Mungu kila kitu kikawa ni chema sasa kinabadilika na kuwa dunia iliyolaaniwa Mwanzo 3;17……. Ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako,uadui na chuki vikaingia katika ulimwengu, viumbe vilivyoumbwa katika ukamilifu vikabadilika na kuiona matokeo ya aanguko ikiwapelekea laana. Dunia nzima ikapoteza maana yake dhambi ikaingia duniani na kwa kuanguka kwake mtu mmoja ulimwengu wote ukahesabiwa adhabu ya kifo. warumi 5:18,19 Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.

Matokeo ya Shetani kuasi mbinguni yameipelekea dunia kuwa si tena mahali panapotamanika, dunia imepoteza kabisa maana yake, dunia imekuwa tena si mahali ambapo bado watu wanatamani kukaa dunia imepoteza tumaini. Matukio makubwa na ya kutisha yameuteka ulimwengu, ajali, vifo, vita, njaa, matetemeko ya ardhi, uasi dhidi ya sheria ya Mungu, chuki kati ya ndugu, jamaa, marafiki, wenzi, nk nk. Dunia haitamaniki tena wapendwa. 

Maisha ya mwanadamu yamegubikwa na dhambi kila siku, huzuni, majonzi, misiba, vilio njaa na shida za kila namna. Watu hawajui wafanye nini, hawajui waende wapi hawajui wakimbilie wapi, watu hawaoni tena faraja kutoka kwa ndugu zao jamaa zao hata watu wao wa karibu nao ndio wamekuwa ni wasaliti kwao kila siku. Dunia imekuwa si tena mahali salama kwao

JE UNAFANYA NINI UNAPOJIKUTA MWENYEWE??
Pamoja na dunia kulaaniwa na dhumuni lake kubadilika kabisa kutoka katika ule mpango wa awali wa Mungu lakini bado Mungu hakumwacha mwanadamu awe pekee yake. Hata pale Adam na Hawa walipoanguka kwa kula tunda bado neema ya Mungu ilikuwa juu yao naye Mungu alilazimika kutoa kafara ya mwanakondoo ili iwe kipatanisho kati ya mwanadamu mdhambi na Mungu muumbaji, bado ngozi yake ilitumika kuficha aibu ya uchi wa mwanadamu aliyekimbia kujificha pia akaweka uadui kati ya mwanadmu na nyoka (shetani) mwanzo 3:15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.

Upendo wa Mungu alio mwingi kwa wanadamu wote bado ulikuwa juu ya mwanadamu mdhambi, na kwa sababu hiyo bado akaona haitoshi kuthibitisha upendo huo hata kumtoa mwanawe pekee ili kuleta ukombozi kwa dunia yote iliyoanguka. Yohana 3:16 wa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Ni kwa sababu ya upendo mwingi wa Mungu hata alidiriki kumtuma mwanawe pekee Yesu Kristo kuja kufa msalabani ili kuleta ondoleo la dhambi, ili kuleta faraja kwao wenye huzuni, ili kuleta tumaini kwao wapotezao tumaini, ili kuleta ukombozi kwao wapoteao, ili kuleta amani kwao wachukianao ili kuleta furaha kwao wahuzunikao.

Kwa upendo huo ilimlazimu Mwana wa Mungu kupitia kifo cha aibu, kifo cha laana, kifo cha dharau kifo cha ukatili ili sisi tupate ondoleo la dhambi na ukombozi kwa ajili ya maisha yetu. Alikubali kuchukua dhambi zetu na kujitwika, alikubali kudharauliwa kwa ajili yetu, alikubali kuudhiwa kwa ajili ya ukombozi wetu alikubali kubeba aibu yetu na adhabu ya amani yetu iliwekwa juu yake Isaya 53:3,4 Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

Ni kupitia kifo cha msalaba ndipo Kristo alipoleta ondoleo la dhambi kwao wamwaminio. Ilimpasa kupitia kifo cha msalaba ili kupatanisha ulimwengu na mbingu, kumpatanisha mwanadamu mdhambi na Mungu mkamilifu. Wakolosai 1:20 kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.


SIMAMA TAZAMA KALVARI
Ni kupitia kalvari Kristo alitupatanisha na Mungu, “uniangalie atwambia, Yesu aliye tufia msalabani ni uzima, hapa utaipata uzima.. kutazama kalwari, kutazama kalwari ni kupewa kuishi kutazama mti”.. hata ijapo tunapitia magumu kiasi gani, hata ijapo dunia imepotea kiasi gani, hata ijapo dunia imepoteza tumaini bado tumaini letu lipo kwake Kristo. Ni kwa kutazama msalaba twapata tumaini, ni kwa kutazama msalaba twapata ondoleo la dhambi, ni kwa kutazama msalaba twapata faraja, kupitia msalaba twapata amani, kupitia msalaba twapata wokovu wa maisha yetu maana ni kupitia msalaba Kristo alifanyika kafara ya milele. Wakolosai 2:14,15akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.

Usikatishwe tamaa wala usizuiliwe na jambo lolote, tumaini lako liweke kwa Kristo pekee. Simama tazama kalvari ukutane na Kristo yeye aliyeichukua aibu yetu, yeye alikubali kudharauliwa kwa ajili ya wokovu wangu na wako waebrania 12:2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

Ni kuptia msalaba hao wamwaminio wataokolewa lakini kwao wapoteao ni upuuzi…….. 1Wakorintho 1:18 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

BWANA AWABARIKI

By Pierre de' Jefter
0783167164
pierredejr2000@gmail.com

UNABII WA MIAKA 2300 sehemu ya 1

UNABII WA MIAKA 2300
(sehemu ya kwanza)

Daniel 8:13, 14.... 13, Ndipo niamsikia mtakatifu mmoja akinena na mtakatifu mwingine akamuuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lin, kukanyagisha patakatifu na jeshi? 14, Akamwambia, Hata nyakati za jioni asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.

Ni katika kipindi cha utawala wa Belshaza mfalme wa Babeli mwana wa mfalme Nebukadneza (Daniel 5:2) ndipo Daniel anaoneshwa maono haya Daniel 8:1 Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake mfalme Belshaza maono yalinitokea mimi, naam, mimi Danieli, baada ya yaliyonitokeahapo kwanza. Akiwa katika wilaya ya Elimu, shushani ngomeni katika mto ulai huko Babeli
Mwanzo wa njozi ya Danieli anaoneshwa kondoo mwenye pembe mbili akisimama na kutawala dunia akisukuma upande wa magharibi na kaskazini na kusini (Daniel 8:3, 4). Kisha anaona beberu akiinuka upande wa mashariki akiwa na pembe mashuhuri kati ya macho (Daniel 8:5). (kwa faida ya msomaji pembe katika unabii huwakilisha ufalme au utawala). Akamkaribia Yule kondoo akamkasirikia kwa ghadhabu nyingi naye akampiga hata kuvunja pembe zake, akamwangusha chini hata kumkanyaga-kanyaga

Baadaye ile pembe ikavunjika kwa kujitukuza hata zikatokea pembe nne zikaielekea pepo nne za mbingu nazo zikatwala kwa kipindi Fulani (Daniel 8:8). Daniel 8:9 Na katika moja ya hizo pembe ilitokea pembe ndogo,iliyokuwa sana, upande wa kusini, na upande wa magharibina upande wan chi ya uzuri. Pia katika fungu la 23; Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo.........atasimama. Hii humaaniasha wakati wa mwisho wa utawala wa falme nne zilizoinuka kutoka kwa Yule beberu ndipo utainuka tena ufalme mwingine unaowakilishwa na pembe ndogo, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo.

Daniel 8:10-14 Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbingun ; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na nyota ikazikanyaga. Naam ikajitukuza hata juu ya aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini. Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa. Ndipo niamsikia mtakatifu mmoja akinena na mtakatifu mwingine akamuuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lin, kukanyagisha patakatifu na jeshi? Akamwambia, Hata nyakati za jioni asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.
Kuinuka kwa pembe hii ndogo na matendo yake ndiko kunamhuzunisha mtakatifu mmoja na hivyo inampelekea kutaka kujua hatima ya haya yote. Nayo ni nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu (2300).

Nini tafsiri yake miaka hii 2300??
Katika sura ya Daniel 8:14 tunaambiwa matukio haya yatachukua muda nyakati za jioni na asubuhi 2300 lakini hatuambiwi chochote kuhusu mwanzo wala mwisho wake.
Katika kuelewa tafsiri hii lazima tuelewe mambo yafuatayo.

1. nyakati za jioni na asubuhi ni sawa na siku nzima amabyo pia huanza jioni hata jioni. Mwanzo 1:5............ ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. kwahiyo nyakati za jioni na asubuhi 2300 ni sawa na siku kamili 2300

2. Katika unabii siku moja ni sawa na mwaka mmoja Ezekiel 4:6.........siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza kwahiyo siku 2300 za kiunabii ni sawa na miaka iliyokamilika 2300.. Hivyo tunasema ili haya yote yafikie mwisho ni mpaka kukamilika kwa miaka 2300.

3. Unabii wa miaka 2300 ndio unabii mrefu kwenye biblia kuliko mengine yote, hivyo unabii mwingine kama vile miaka 1260, majuma 70, miaka 1335 na 1290 zote huangukia kwenye miaka 2300.

Mwanzo wa miaka hii ni upi?
Mwanzo wa miaka hii tunaelewa kwa kuelewa mianzo ya majuma 70 katika Daniel 9:24. Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu.........,25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kujenga upya mji wa Yerusalemu..... kutakuwa na majuma saba.............

Majuma sabini ni sawa na miaka 490. 70x7=490. Hii hutuambia kuwa kulikuwa na miaka 490 ulioamriwa juu ya taifa la Israeli. Amri juu ya ujenzi wa mji wa yerusalemu ulitolewa na mfalme Artashasta mfalme wa uajemi mnamo mwaka wa 457 K.K (kabla ya kristo) Ezra 7:21-26 Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa amri wote wenye kutunza hazina.....hata kiasi cha cha talanta mia za fedha .... kila neon litakaloamriwa na Mungu wa mbinguni, na litendeke halisi kwa ajili ya ya nyumba ya Mungu wa mbinguni........ Kuanzia mwaka wa 457 hitimisho la miaka 490 au majuma 70 hufikia 34 B.K (baada ya Kristo), (kumbuka kuna mwaka kutoka 0-1)....katika miaka 2300 baada ya kukamilika kwa miaka 490 tunasalia na miaka 1810. 
490+1810=2300.na 
Siku 2300 zilioneka kuanza wakati amri ya Artashasta kwa ajili ya urejeshwaji wa na ujenzi wa Yerusalemu ilipotolewa majira ya kipupwe ya mwaka 457 K.K. Kwahiyo mwanzo wa miaka 2300 ni mwaka 457 B.K na huishia mwaka 1844 B.K.

Bwana atubariki tukutane sehemu ya pili kujifunza matukio makubwa yaliyotabiriwa na kutokea katika kipindi hiki cha miaka 2300.

By Pierre de' Jefter
0783167164
pierredejr2000@gmail.com

UNABII NI NINI??

                            UNABII NI NINI??

2petro 1:19, Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi,ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza.......

Mara nyingi kumekuwepo na maswali meni mbalimbali ambayo wengi wetu tumejiuliza kuhusu unabii, na wengi pia tumeshindwa kuelewa unabii, wengine hata wamediriki kuyakataa mafundisho ya unabii katika makanisa yao kwa sababu ya kutokueleweka kwake na baadhi wamesema muda bado wa kujifunza unabii kwa kuwa ni maandiko maalum kwa ajili ya kipindi cha mwisho ( je kipindi cha mwisho ni kipi???).
Unabii ni mafunuo ya Mungu aliyoyaleta kwa wanadamu kwa njia ya maono kupitia watu maalum (manabii) walioteuliwa na Mungu kwa ajili ya kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii au watu husikaYeremia 1:5, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Unabii haukuletwa wala kufasiriwa kwa mapenzi ya mwanadamu yeyote, bali alipaswa kufikisha ujumbe kama alivyopokea kwa Mungu.2petro 1:20,21 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya wanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho mtakatifu. Mapenzi ya Mungu yalifika kama alivyo kusudia yeye mwenyewe. Yeremia 1:6 ....... maana utakwenda kwa kila mtu nitakaetuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru

Makusudi ya Mungu kuwateua manabii na kuwatuma kupeleka ujumbe ulikuwa ni kupeleka maonyo, mafundisho, maongozo nk. 2timotheo 3:16,17 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao,  na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.maandiko yote katika Biblia ni hai kwa kuwa yanashuhudiwa kuwa yana pumzi ya Mungu na hivyo yafaa kwa kuelimisha na kuongoza katika haki na kweli.

UNABII ULILETWA KAMA UFUNUO/MAONO
Unabii wa Mungu uliletwa kwa wanadamu (manabii) kama maono au njozi lakini pia hawakuacha kuoneshwa tafsiri yake. Ufunuo 1:1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana; mtiririko wa maono haya ulianza kwa Mungu, akapewa Yesu kupitia mkono wa malaika unafika kwa Yohana. Malaki1:1 Ufunuo wa neno la Bwana kwa Israeli kwa mkono wa Malaki,


KWANINI TUSOME UNABII??
Imetupasa kusoma unabii kwakuwa yote yaliyotabiriwa hayana budi kutokea upesi na hivyo kuwa wanafunzi wa unabii kunatupelekea kuelewa makusudio ya Mungu kwetu hata leo  Ufunuo 1:1..... Awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi....... kila kilichotabiriwa katika Biblia ni lazima kitatimia wala hakitapita kamwe. Mathayo 5:18 ..... mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka hata yote yatimie.

wana heri hao wazisomao na kuyashika maneno ya  unabii. Ufunuo 1:3 Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu. Kinyume cha neno heri ni ole.... neno ole humaanisha onyo, kwahiyo kinye cha neno onyo ni bahati njema/nzuri. Tangazo la bahati njema Mungu anaitoa kwa hao wasomao maneno ya unabii na si kuyasoma tu bali pia kuyashika ikiwa na maana kuwa tuyasome maneno ya unabii huu na kuyashika/ kuyatii maagizo hayo, kwa sababu wakati u karibu.

Imetupasa pia kuyasoma na kuyashika maneno ya unabii kwa sababu yote yaliyotabiriwa sasa twayaona yakitokea. Ni bahati tu kwao hao wanayoyaelewa hayo yaliyosemwa kwa kuwa ndio nyakati zile zilizonenwa kuwa ni za mwisho.Daniel 12:9 Akasema enenda zako, Danieli  maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho. Na hivyo imetuapsa kuachana na dhana zisemazo ya kuwa unabii ni mgumu haueleweki au hakuna mwanadamu awezaye kuelewa kitabu cha unabii au hata hao wasemao wakati wa kujifunza unabii bado haujafika. Wana heri hao wazisomao na kuyatii hayo......... wakati wa kusoma unabii ndio sasa
Wapo manabii wengi kwenye Biblia kama vile Eliya, Elisha, Samwel, Daniel, Yohana, Isaya nk. Wapo walioandika vitabu katika Biblia wengine wameelezewa tu kama walikuwepo. Katika Biblia kuna vitabu 18 vya unabii vikiwa katika mgawanyiko wa unabii mkubwa na unabii mdogo

Vitabu hivyo ni

Unabii mkubwa

1, Ufunuo 2, Danieli 3, Isaya 4, Ezekiel 5, Yeremia

Unabii mdogo

1, Hosea 2, Yoeli 3, Amosi 4, Obadia 5, Yona 6, Mika 7, Nahumu 8, Sefania 9, Hagai 10, Zekaria 11, Habakuki 12, Malaki 13, maombolezo ya Yeremia
Utoafauti unaofanya kuwa kwa unabii mdogo na mkubwa sio waandishi kama tutakavyodhani la! Manabii wote ni sawa isipokuwa utofauti wa udogo na ukubwa ni ujumbe. Wengine huitwa manabii wakubwa kwa sababu ya ukubwa wa ujumbe na wengine huitwa wadogo kwa sababu ya udogo wa 
ujumbe wao.

NABII NI NANI??
Nabii ni mteuliwa wa Mungu aliyeitwa kupeleka ujumbe kwa watumwa/ watu wa Mungu kama vile Yohana, Yeremia Ezekiel nk.,. Wengine waliitwa kufunua siri zilizofichwa kama vile Danieli. Nabii hakutokea tu kusikojulikana au mtu yeyote kutokea na kujitangaza kuwa yeye ni nabii kama ilivyo kwetu leo. Nabii aliandaliwa na Mungu na alitumwa na Mungu yeremia 1:5

Onyo juu ya manabii wa uongo

Ieleweke kuwa katika kila kilicho halisi (valid) lazima kuna batili (invalid). Mungu kwa kutambua hilo alijua pia kwa kuwepo kwa manabii wake wa kweli lazima watakuwepo na manabii wa uongo na hivyo hakuacha kutuonya. 2petro 2:1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo,.......... Mathayo 24:11, Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. Kipindi cha mwisho kilitabiriwa kuwa manabii wengi wa uongo watatokea wakidanganya yumkini hata walio wateule, na hivyo imetupasa kusimama 
upande wa Kristo ili atuokoe na nguvu za upotevu
Tutawatambuaje?

Mathayo 7:15,16 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia  wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao............
1yohana 4:1-3 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani............. kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu............ Mungu aliyajua haya mapema wengi watatokea wakijiita wao ni manabii wakijaribu hata kutabiri mambo mengi ikiwemo habari ya kurudi kwa Yesu. Biblia imetuonya juu ya manabii hao na wala tusiwaamini hao wajiitao manabii bali tuwapime kwanza kwa maandiko, je wamekamilika hata katika AMRI za Mungu??? Nabii wa kweli wa Mungu hawezi kufundisha kuwa amri za Mungu hazina umuhimu, nabii wa kweli wa Mungu hawezi kutabiri kilicho kinyume na Biblia takatifu.


Akhsanteni BWANA awabariki
By Pierre de' Jefter
0783167164
pierredejr2000@gmail.com