UNABII NI NINI??
2petro 1:19, Nasi tuna lile neno la unabii lililo
imara zaidi,ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza.......
Mara nyingi kumekuwepo na maswali meni
mbalimbali ambayo wengi wetu tumejiuliza kuhusu unabii, na wengi pia
tumeshindwa kuelewa unabii, wengine hata wamediriki kuyakataa mafundisho ya
unabii katika makanisa yao kwa sababu ya kutokueleweka kwake na baadhi wamesema
muda bado wa kujifunza unabii kwa kuwa ni maandiko maalum kwa ajili ya kipindi
cha mwisho ( je kipindi cha mwisho ni kipi???).
Unabii ni mafunuo ya Mungu aliyoyaleta
kwa wanadamu kwa njia ya maono kupitia watu maalum (manabii) walioteuliwa na
Mungu kwa ajili ya kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii au watu husika. Yeremia 1:5, Kabla sijakuumba katika tumbo
nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa
mataifa.
Unabii haukuletwa wala kufasiriwa kwa
mapenzi ya mwanadamu yeyote, bali alipaswa kufikisha ujumbe kama alivyopokea
kwa Mungu.2petro 1:20,21 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika
maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii
haukuletwa popote kwa mapenzi ya wanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka
kwa Mungu, wakiongozwa na Roho mtakatifu. Mapenzi ya Mungu yalifika
kama alivyo kusudia yeye mwenyewe. Yeremia 1:6 ....... maana utakwenda kwa kila
mtu nitakaetuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru
Makusudi ya Mungu kuwateua manabii na
kuwatuma kupeleka ujumbe ulikuwa ni kupeleka maonyo, mafundisho, maongozo nk. 2timotheo
3:16,17 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa
kuwaonya watu makosa yao, na kwa
kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili,
amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.maandiko yote katika Biblia
ni hai kwa kuwa yanashuhudiwa kuwa yana pumzi ya Mungu na hivyo yafaa kwa
kuelimisha na kuongoza katika haki na kweli.
UNABII
ULILETWA KAMA UFUNUO/MAONO
Unabii wa Mungu uliletwa kwa wanadamu
(manabii) kama maono au njozi lakini pia hawakuacha kuoneshwa tafsiri yake. Ufunuo
1:1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo
ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika
akamwonyesha mtumwa wake Yohana; mtiririko wa maono haya ulianza kwa
Mungu, akapewa Yesu kupitia mkono wa malaika unafika kwa Yohana. Malaki1:1
Ufunuo wa neno la Bwana kwa Israeli kwa mkono wa Malaki,
KWANINI
TUSOME UNABII??
Imetupasa kusoma unabii kwakuwa yote
yaliyotabiriwa hayana budi kutokea upesi na hivyo kuwa wanafunzi wa unabii
kunatupelekea kuelewa makusudio ya Mungu kwetu hata leo Ufunuo 1:1..... Awaonyeshe watumwa wake
mambo ambayo hayana budi kuwako upesi....... kila kilichotabiriwa
katika Biblia ni lazima kitatimia wala hakitapita kamwe. Mathayo 5:18 ..... mpaka mbingu
na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka hata
yote yatimie.
wana heri hao wazisomao na kuyashika
maneno ya unabii. Ufunuo 1:3 Heri asomaye na wao
wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana
wakati u karibu. Kinyume cha neno heri ni ole.... neno ole humaanisha
onyo, kwahiyo kinye cha neno onyo ni bahati njema/nzuri. Tangazo la bahati
njema Mungu anaitoa kwa hao wasomao maneno ya unabii na si kuyasoma tu bali pia
kuyashika ikiwa na maana kuwa tuyasome maneno ya unabii huu na kuyashika/
kuyatii maagizo hayo, kwa sababu wakati u karibu.
Imetupasa pia kuyasoma na kuyashika
maneno ya unabii kwa sababu yote yaliyotabiriwa sasa twayaona yakitokea. Ni
bahati tu kwao hao wanayoyaelewa hayo yaliyosemwa kwa kuwa ndio nyakati zile
zilizonenwa kuwa ni za mwisho.Daniel 12:9 Akasema enenda zako,
Danieli maana maneno haya yamefungwa, na
kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho. Na hivyo imetuapsa kuachana na
dhana zisemazo ya kuwa unabii ni mgumu haueleweki au hakuna mwanadamu awezaye
kuelewa kitabu cha unabii au hata hao wasemao wakati wa kujifunza unabii bado
haujafika. Wana heri hao wazisomao na kuyatii hayo......... wakati wa kusoma
unabii ndio sasa
Wapo manabii wengi kwenye Biblia kama vile
Eliya, Elisha, Samwel, Daniel, Yohana, Isaya nk. Wapo walioandika vitabu katika
Biblia wengine wameelezewa tu kama walikuwepo. Katika Biblia kuna vitabu 18 vya
unabii vikiwa katika mgawanyiko wa unabii mkubwa na unabii mdogo.
Vitabu hivyo
ni
Unabii
mkubwa
1, Ufunuo 2, Danieli 3, Isaya 4, Ezekiel
5, Yeremia
Unabii
mdogo
1, Hosea 2, Yoeli 3, Amosi 4, Obadia 5,
Yona 6, Mika 7, Nahumu 8, Sefania 9, Hagai 10, Zekaria 11, Habakuki 12, Malaki
13, maombolezo ya Yeremia
Utoafauti unaofanya kuwa kwa unabii mdogo
na mkubwa sio waandishi kama tutakavyodhani la! Manabii wote ni sawa isipokuwa
utofauti wa udogo na ukubwa ni ujumbe. Wengine huitwa manabii wakubwa kwa
sababu ya ukubwa wa ujumbe na wengine huitwa wadogo kwa sababu ya udogo wa
ujumbe wao.
NABII
NI NANI??
Nabii ni mteuliwa wa Mungu aliyeitwa
kupeleka ujumbe kwa watumwa/ watu wa Mungu kama vile Yohana, Yeremia Ezekiel
nk.,. Wengine waliitwa kufunua siri zilizofichwa kama vile Danieli. Nabii
hakutokea tu kusikojulikana au mtu yeyote kutokea na kujitangaza kuwa yeye ni
nabii kama ilivyo kwetu leo. Nabii aliandaliwa na Mungu na alitumwa na Mungu yeremia
1:5
Onyo
juu ya manabii wa uongo
Ieleweke kuwa katika kila kilicho halisi
(valid) lazima kuna batili (invalid). Mungu kwa kutambua hilo alijua pia kwa
kuwepo kwa manabii wake wa kweli lazima watakuwepo na manabii wa uongo na hivyo
hakuacha kutuonya. 2petro 2:1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama
vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo,.......... Mathayo 24:11, Na
manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. Kipindi cha
mwisho kilitabiriwa kuwa manabii wengi wa uongo watatokea wakidanganya yumkini
hata walio wateule, na hivyo imetupasa kusimama
upande wa Kristo ili atuokoe na
nguvu za upotevu
Tutawatambuaje?
Mathayo 7:15,16 Jihadharini na manabii wa uongo,
watu wanaowajia wamevaa mavazi ya
kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda
yao............
1yohana 4:1-3 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali
zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo
wengi wametokea duniani............. kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na
Mungu............ Mungu aliyajua haya
mapema wengi watatokea wakijiita wao ni manabii wakijaribu hata kutabiri mambo
mengi ikiwemo habari ya kurudi kwa Yesu. Biblia imetuonya juu ya manabii hao na
wala tusiwaamini hao wajiitao manabii bali tuwapime kwanza kwa maandiko, je
wamekamilika hata katika AMRI za Mungu??? Nabii wa kweli wa Mungu hawezi
kufundisha kuwa amri za Mungu hazina umuhimu, nabii wa kweli wa Mungu hawezi
kutabiri kilicho kinyume na Biblia takatifu.
Akhsanteni BWANA awabariki
By Pierre de' Jefter
0783167164
pierredejr2000@gmail.com
2petro 1:19, Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi,ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza.......
Mara nyingi kumekuwepo na maswali meni mbalimbali ambayo wengi wetu tumejiuliza kuhusu unabii, na wengi pia tumeshindwa kuelewa unabii, wengine hata wamediriki kuyakataa mafundisho ya unabii katika makanisa yao kwa sababu ya kutokueleweka kwake na baadhi wamesema muda bado wa kujifunza unabii kwa kuwa ni maandiko maalum kwa ajili ya kipindi cha mwisho ( je kipindi cha mwisho ni kipi???).
Unabii ni mafunuo ya Mungu aliyoyaleta kwa wanadamu kwa njia ya maono kupitia watu maalum (manabii) walioteuliwa na Mungu kwa ajili ya kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii au watu husika. Yeremia 1:5, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Unabii haukuletwa wala kufasiriwa kwa mapenzi ya mwanadamu yeyote, bali alipaswa kufikisha ujumbe kama alivyopokea kwa Mungu.2petro 1:20,21 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya wanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho mtakatifu. Mapenzi ya Mungu yalifika kama alivyo kusudia yeye mwenyewe. Yeremia 1:6 ....... maana utakwenda kwa kila mtu nitakaetuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru
Makusudi ya Mungu kuwateua manabii na
kuwatuma kupeleka ujumbe ulikuwa ni kupeleka maonyo, mafundisho, maongozo nk. 2timotheo
3:16,17 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa
kuwaonya watu makosa yao, na kwa
kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili,
amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.maandiko yote katika Biblia
ni hai kwa kuwa yanashuhudiwa kuwa yana pumzi ya Mungu na hivyo yafaa kwa
kuelimisha na kuongoza katika haki na kweli.
UNABII
ULILETWA KAMA UFUNUO/MAONO
Unabii wa Mungu uliletwa kwa wanadamu
(manabii) kama maono au njozi lakini pia hawakuacha kuoneshwa tafsiri yake. Ufunuo
1:1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo
ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika
akamwonyesha mtumwa wake Yohana; mtiririko wa maono haya ulianza kwa
Mungu, akapewa Yesu kupitia mkono wa malaika unafika kwa Yohana. Malaki1:1
Ufunuo wa neno la Bwana kwa Israeli kwa mkono wa Malaki,
KWANINI
TUSOME UNABII??
Imetupasa kusoma unabii kwakuwa yote
yaliyotabiriwa hayana budi kutokea upesi na hivyo kuwa wanafunzi wa unabii
kunatupelekea kuelewa makusudio ya Mungu kwetu hata leo Ufunuo 1:1..... Awaonyeshe watumwa wake
mambo ambayo hayana budi kuwako upesi....... kila kilichotabiriwa
katika Biblia ni lazima kitatimia wala hakitapita kamwe. Mathayo 5:18 ..... mpaka mbingu
na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka hata
yote yatimie.
wana heri hao wazisomao na kuyashika
maneno ya unabii. Ufunuo 1:3 Heri asomaye na wao
wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana
wakati u karibu. Kinyume cha neno heri ni ole.... neno ole humaanisha
onyo, kwahiyo kinye cha neno onyo ni bahati njema/nzuri. Tangazo la bahati
njema Mungu anaitoa kwa hao wasomao maneno ya unabii na si kuyasoma tu bali pia
kuyashika ikiwa na maana kuwa tuyasome maneno ya unabii huu na kuyashika/
kuyatii maagizo hayo, kwa sababu wakati u karibu.
Imetupasa pia kuyasoma na kuyashika maneno ya unabii kwa sababu yote yaliyotabiriwa sasa twayaona yakitokea. Ni bahati tu kwao hao wanayoyaelewa hayo yaliyosemwa kwa kuwa ndio nyakati zile zilizonenwa kuwa ni za mwisho.Daniel 12:9 Akasema enenda zako, Danieli maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho. Na hivyo imetuapsa kuachana na dhana zisemazo ya kuwa unabii ni mgumu haueleweki au hakuna mwanadamu awezaye kuelewa kitabu cha unabii au hata hao wasemao wakati wa kujifunza unabii bado haujafika. Wana heri hao wazisomao na kuyatii hayo......... wakati wa kusoma unabii ndio sasa
Wapo manabii wengi kwenye Biblia kama vile Eliya, Elisha, Samwel, Daniel, Yohana, Isaya nk. Wapo walioandika vitabu katika Biblia wengine wameelezewa tu kama walikuwepo. Katika Biblia kuna vitabu 18 vya unabii vikiwa katika mgawanyiko wa unabii mkubwa na unabii mdogo.
Unabii
mkubwa
1, Ufunuo 2, Danieli 3, Isaya 4, Ezekiel 5, Yeremia
Unabii
mdogo
1, Hosea 2, Yoeli 3, Amosi 4, Obadia 5, Yona 6, Mika 7, Nahumu 8, Sefania 9, Hagai 10, Zekaria 11, Habakuki 12, Malaki 13, maombolezo ya Yeremia
Utoafauti unaofanya kuwa kwa unabii mdogo na mkubwa sio waandishi kama tutakavyodhani la! Manabii wote ni sawa isipokuwa utofauti wa udogo na ukubwa ni ujumbe. Wengine huitwa manabii wakubwa kwa sababu ya ukubwa wa ujumbe na wengine huitwa wadogo kwa sababu ya udogo wa
ujumbe wao.
Nabii ni mteuliwa wa Mungu aliyeitwa kupeleka ujumbe kwa watumwa/ watu wa Mungu kama vile Yohana, Yeremia Ezekiel nk.,. Wengine waliitwa kufunua siri zilizofichwa kama vile Danieli. Nabii hakutokea tu kusikojulikana au mtu yeyote kutokea na kujitangaza kuwa yeye ni nabii kama ilivyo kwetu leo. Nabii aliandaliwa na Mungu na alitumwa na Mungu yeremia 1:5
Onyo
juu ya manabii wa uongo
Ieleweke kuwa katika kila kilicho halisi (valid) lazima kuna batili (invalid). Mungu kwa kutambua hilo alijua pia kwa kuwepo kwa manabii wake wa kweli lazima watakuwepo na manabii wa uongo na hivyo hakuacha kutuonya. 2petro 2:1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo,.......... Mathayo 24:11, Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. Kipindi cha mwisho kilitabiriwa kuwa manabii wengi wa uongo watatokea wakidanganya yumkini hata walio wateule, na hivyo imetupasa kusimama
upande wa Kristo ili atuokoe na nguvu za upotevu
Tutawatambuaje?
Mathayo 7:15,16 Jihadharini na manabii wa uongo,
watu wanaowajia wamevaa mavazi ya
kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda
yao............
1yohana 4:1-3 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali
zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo
wengi wametokea duniani............. kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na
Mungu............ Mungu aliyajua haya
mapema wengi watatokea wakijiita wao ni manabii wakijaribu hata kutabiri mambo
mengi ikiwemo habari ya kurudi kwa Yesu. Biblia imetuonya juu ya manabii hao na
wala tusiwaamini hao wajiitao manabii bali tuwapime kwanza kwa maandiko, je
wamekamilika hata katika AMRI za Mungu??? Nabii wa kweli wa Mungu hawezi
kufundisha kuwa amri za Mungu hazina umuhimu, nabii wa kweli wa Mungu hawezi
kutabiri kilicho kinyume na Biblia takatifu.
Akhsanteni BWANA awabariki
By Pierre de' Jefter
0783167164
pierredejr2000@gmail.com
LAZARO ABEL ni kweli asomaye na afahamu ibada halisi na bandia
ReplyDelete